K.I.B.A. K.I.B.A. -- Klubo Internacia de Bao-Amantoj
New! Usisahau kusajili kituo cha video ya Bao kwenye YouTube.
Mkutano ujao 17/19 - 05 - 2024: Play (Festival del Gioco) - Modena (Italia)

Kanuni za kuandika mchezo

Wachezaji
Mchezaji wa kwanza kucheza anaitwa Kusini, mshindani wake anaitwa Kaskazini.

Mashimo ya mchezaji wa Kusini
Mstari wa mbele wa mashimo ya Kusini umeonyeshwa kwa herufi A.
Mstari wa nyuma wa mashimo ya Kusini umeonyeshwa kwa herufi B.

Mashimo ya mchezaji wa Kaskazini
Mstari wa mbele wa mashimo ya Kaskazini umeonyeshwa kwa herufi a.
Mstari wa nyuma wa mashimo ya Kaskazini umeonyeshwa kwa alama b.

Mashimo kwa kila mstari yamepewa namba 1 hadi 8, kuanzia upande wa kushoto wa kila mchezaji.

Kwa hiyo:
nyumba ya mchezaji wa kusini imeonyeshwa kwa A5 ambapo ile ya mchezaji wa kaskazini ni imeonyeshwa kwa a5.
Vichwa ni: A1, A8, a1 na a8,
kimbi ni: A2, A7, a2 na a7.

Mizunguko
Mizunguko imeonyeshwa kwa mstari ('A', 'B', 'a', 'b') na namba ya shimo kunakoanzia mzunguko (1-8).

Uelekeo wa mzunguko umeonyeshwa kwa alama < au >.
< ikiwa na maana ya kwenda upande wa kushoto wa mchezaji,
> ikiwa na maana ya kwenda upande wa kulia wa mchezaji.
# ikiwa na maana ya Bao hamna.

Mfano:
A4<
ina maana kwamba mchezaji wa Kusini anachukua kete zilizomo ndani ya shimo A4 akaelekea upande wake wa kulia.


Kama mchezaji anaamua kucheza nyumba yake alama ya + (kujumlisha) inaongezwa kwenye mzunguko.
Mfano:
A3>+
ina maana kwamba mchezaji wa Kusini anachukua kete zilizomo ndani ya shimo A3 akaelekea upande wake wa kulia, akifika nyumba yake, A5, anaicheza.


Kutakata (au kutakasa) kunaonyeshwa kwa alama ya (nyota) *,
kutakatia kunaonyeshwa kwa alama mbili za nyota **.

Wakati wa kunamua si lazima kuandika herufi mistari yaani ('A' au 'a').

Kama shimo, mchezaji analokula, ni kichwa au kimbi alama ya mwelekeo ('>' au '<') inaweza kuachwa.

Kumbuka kwamba ishara za mwelekeo zinahusiana na mchezaji tu, yaani inaonyesha upande unakoelekea mkono wa mchezaji baada ya kutia kete ya kwanza wakati wa kunamua au baada ya kula kete wakati wa mtaji.

Kwa hiyo mchezaji akila wakati wa kunamua mwelekeo unaonyesha upande wake wa kulia ('>') au wa kushoto ('<') wa kichwa kilichochaguliwa kuanza kutia kete.

Maandiko ya mchezo yana kichwa chenye maelezo ya mchezo na mstari mmoja kwa kila jozi ya mizunguko.
Jina la mchezaji wa Kusini linaandikwa kwa herufi kubwa, lile la mchezaji wa Kaskazini linaandikwa kwa herufi ndogo.
Mstari wa jozi ya mizunguko unaanza kwa namba ya mzunguko, nukta pacha, nafasi, mzunguko wa Kusini, mzunguko wa Kaskazini na nuktamkato.
Mfano:
1: A6<* a5>;
ina maana kwamba mchezaji wa Kusini alitakata kwa kuchukua kete zilizomo ndani ya shimo A6 kuelekea upande wake wa kushoto, ambapo mchezaji wa Kaskazini alicheza a5 akaelekea upande wake wa kulia.


Tazama mfano wa maandiko ya mchezo.
© Nino Vessella (w3.css) ×